• HABARI MPYA

  Sunday, January 10, 2021

  HAALAND APIGA MBILI DORTMUND YAICHAPA RB LEIPZIG 3-0


  MABAO ya Erling Haaland mawili na Jadon Sancho moja usiku wa jana yaliipa Borussia Dortmund ushindi wa 3-1 dhidi ya RB Leipzig ambayo bao lake lilifungwa na mtokea benchi Alexander Sorloth katika mchezo wa Bundesliga Uwanja wa Red Bull Aren.
  Leipzig walihitaji ushindi ili kupanda kileleni kufuatia Bayern Munich kufungwa 3-2 na Borussia Moenchengladbach Ijumaa, hivyo sasa wanaendelea kuwa nyuma ya mabingwa hao watetezi kwa pointi moja baada yua kipigo hicho cha kwanza cha nyumbani msimu huu.
  Dortmund wanasogea nafasi ya nne wakizidiwa pointi tatu na Leipzig baada ya ushindi huo wa tatu katika mechi nne chini ya kocha mpya, Edin Terzic 


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAALAND APIGA MBILI DORTMUND YAICHAPA RB LEIPZIG 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top