• HABARI MPYA

  Sunday, January 24, 2021

  TAIFA STARS YAICHAPA NAMIBIA 1-0 NA KUFUFUA MATUMAINI YA KUSONGA MBELE FAINALI ZA CHAN CAMEROON

  TANZANIA imefufua matumaini ya kwenda Robo Fainali ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Namibia, bao pekee la kiungo Farid Mussa Malik dakika ya 65 akimalizia pasi ya mchezaji mwenzake wa Yanga, Ditram Nchimbi katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Limbe, Cameroon.
  Baada ya sare ya 1-1 katika mchezo uliotangulia jana jioni, sasa Guinea na Zambia zinalingana kwa pointi, nne kila timu zikifuatiwa na Tanzania yenye pointi tatu, wakati Namibia imeaga mashindano baada ya kufungwa mechi zote mbili za mwanzo.

  Sasa Tanzania watatakiwa kushinda mechi yao ya mwisho ya kundi hilo dhidi ya Guinea Jumatano Uwanja wa Reunification, Douala ili kwenda Robo Fainali.
  Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Bakari Mwamnyeto, Edward Manyama, Deus Kaseke/ Rajab Athuman dk65, Ayoub Lyanga, Feisal Salumsk, Said Ndemla, Farid Mussa/Baraka Majogoro dk83 na D. Nchimbi.
  Namibia; Kamaijanda Ndisiro, Emilio Martin, Vetunuavi Charles Hambira, Ivan Kamberipa, Aprocious Petrus/ Panduleni Nekundi dk90, Alfeus Handura/ Marcel Papama dk61, Wesley Katjiteo, Absalom Iimbondi, Elmo Kambindu/ Isaskar Gurirab dk60 na Deryl Goagoseb.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YAICHAPA NAMIBIA 1-0 NA KUFUFUA MATUMAINI YA KUSONGA MBELE FAINALI ZA CHAN CAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top