• HABARI MPYA

    Saturday, January 23, 2021

    JONAS MKUDE ATOZWA FAINI YA SH. MILIONI 2 KWA UTOVU WA NIDHAMU SIMBA SC NA KUTAKIWA KUREJEA KAMBINI MARA MOJA

    KAMATI ya Nidhamu ya Klabu ya Simba chini ya Mwenyekiti wake, Suleiman Kova imetangaza hukumu ya kiungo wa klabu hiyo, Jonas Mkude ambaye alisimamishwa na uongozi kwa makosa ya utovu wa nidhamu. 
    Kwa mujibu wa Kova, haya ndiyo makosa matatu aliyokuwa akituhumiwa kuyafanya, pamoja na hukumu zake.


    KOSA LA KWANZA: Kutohudhuria semina elekezi iliyohusisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi. Adhabu yake ni faini ya shilingi milioni moja (1,000,000).
    KOSA LA PILI: Kuchelewa kuingia kambini wakati timu ilipokuwa ikijiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union.  Adhabu aliyopewa ni karipio kali na faini ya shilingi milioni moja (1,000,000) pamoja na kuwekwa katika kipindi cha uangalizi cha miezi sita.
    KOSA LA TATU:  Kutoripoti kambini siku ya 26/12/2020 bila ruhusa. Katika tuhuma hizi, kamati haikumkuta na hatia baada ya kamati kutothibitisha pasipo shaka shitaka hilo.
    MAAGIZO
    Kamati imemtaka Mkude kurejea kambini mara moja kuendelea na mazoezi na asipofanya hivyo atakuwa amefanya tena kosa la utovu wa nidhamu.
    Faini aliyotozwa anatakiwa kuilipa ndanI ya mwezi mmoja.
    Kamati imemtaka Mkude kuomba radhi kwa maandishi ndani ya saa 24. 
    #HukumuYaMkude #JonasMkude #SimbaSC
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JONAS MKUDE ATOZWA FAINI YA SH. MILIONI 2 KWA UTOVU WA NIDHAMU SIMBA SC NA KUTAKIWA KUREJEA KAMBINI MARA MOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top