• HABARI MPYA

  Saturday, January 23, 2021

  SIMBA SC YAMTAMBULISHA MBRAZIL MILTON NIENOV KUWA KOCHA WAKE MPYA WA MAKIPA

  KLABU ya Simba imemtambulisha Mbrazil, Milton Nienov Huyu kuwa kocha wake mpya wa makipa, akichukua nafasi ya Muharami Mohammed 'Shilton' aliyeondolewa mwishoni mwa mwaka jana.
  "Huyu ndio baba yetu katika milingoti mitatu ya Mabingwa wa nchi. Ndie mwenye jukumu la kuhakikisha makipa wetu wanakuwa bora maradufu," imesema taarifa ya Simba SC leo.
  Milton Nienov amewahi kuwa kocha wa makipa wa klabu za Polokwane City, Lamontville Golden Arrows FC, Super Eagles FC, Free State Stars FC za Afrika Kusini na Club de Regatas Vasco da Gama, Sport Club Recifie na Figueirense FC za kwao, Brazil.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAMTAMBULISHA MBRAZIL MILTON NIENOV KUWA KOCHA WAKE MPYA WA MAKIPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top