• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 09, 2021

  SIMBA SC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 ZANZIBAR NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  SIMBA SC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar usiku wa leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Pongezi kwa wafungaji wa mabao hayo, Hassan Dilunga dakika ya sita na Miraj Athumani ‘Madenge’ dakika ya 36 na kwa ushindi huo, Simba SC inamaliza kileleni mwa Kundi B.
  Katika mchezo uliotangulia, mabao ya Erick Kwizera dakika ya 41 na Stephen Sey dakika ya 52 yaliipa ushindi wa 2-0 Namungo FC dhidi ya Jamhuri katika mchezo wa Kundi A.
  Kwa matokeo hayo, Namungo inamaliza nafasi ya pili kwenye kundi hilo na kutinga Nusu Fainali ikiungana na vinara wa kundi, Yanga SC waliomaliza na pointi nne.
  Sasa Namungo FC itamenyana na Simba SC katika Nusu Fainali, wakati Yanga SC watasubiri mshindi wa mechi ya Kundi C kesho baina ya Azam FC na Malindi SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 ZANZIBAR NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top