• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 28, 2021

  MAN UNITED YACHAPWA 2-1 NA SHEFFIELD UNITED NYUMBANI  MANCHESTER United jana wamepoteza nafasi ya kurejea kileleni katika Ligi Kuu ya England baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Sheffield United Uwanja wa Old Trafford.
  Beki Kean Bryan alianza kuwafungia Sheffield dakika ya 23, kabla ya Nahodha wa
  Manchester United, Harry Maguire kuisawazishia timu yake dakika ya 64 na mtokea benchi, Oliver Burke akawafungia wageni bao la ushindi dakika 10 baadaye.
  Manchester United inabaki nafasi ya pili na pointi zake 40 baada ya kucheza mechi 20, ikizidiwa pointi moja na mahasimu wao wa Jiji, Manchester City ambao pia wana mechi moja mkononi 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YACHAPWA 2-1 NA SHEFFIELD UNITED NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top