• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 07, 2021

  MESSI APIGA BARCELONA YAICHAPA ATHLETIC BILBAO 3-2 LA LIGA


  NYOTA Lionel Messi jana amefunga mabao mawili dakika za 38 na 63 kuiwezesha Barcelona kupata ushindi wa 3-2 dhidi ya Athletic Bilbao katika mchezo wa La Liga Uwanja wa San Mames Barria. Bao lingine la Barca lilifungwa na Pedri dakika ya 14, wakati mabao ya Athletic Bilbao yalifungwa na Inaki Williams dakika ya tatu na Iker Muniain dakika ya 90. Ushindi huo unaiosogeza nafasi ya tatu Barcelona ikifikisha pointi 31, sasa ikizidiwa pointi tano na mahasimu wao, Real Madrid baada ya timu zote kucheza mechi 17 na wote wapo nyuma ya Atletico Madrid inayoongoza kwa pointi zake 38 za mechi 15
   

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI APIGA BARCELONA YAICHAPA ATHLETIC BILBAO 3-2 LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top