• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 25, 2021

  YANGA SC YAMTANGAZA MCHEZAJI WAKE WA ZAMANI NIZAR KHALFAN KUWA KOCHA MPYA MSAIDIZI WA MRUNDI KAZE

  KLABU Yanga SC imemtangaza rasmi mchezaji wake wa zamani na kocha wa African Lyon, Nizar Khalfan kuwa kocha mpya Msaidizi wa Mrundi, Cedric Kaze akichujua nafasi ya Juma Mwambusi aliyejiuzulu hivi karibuni kwa sababu za kiafya.
  Kwa mujibu wa Afisa Habari wa timu hiyo Hassan Bumbuli, Nizar amepata nafasi hiyo baada ya kupita kwenye usaili uliofanyika Ijumaa ya Januari 22, mwaka huu.
  Bumbuli amebainisha kuwa kulikuwa na makocha takribani 10 waliojitokeza kuisaka nafasi hiyo na watano walifikia hatua ya mwisho(fainali) akiwemo Salvatory Edward, Maalim Saleh na Omary Kapilima.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YAMTANGAZA MCHEZAJI WAKE WA ZAMANI NIZAR KHALFAN KUWA KOCHA MPYA MSAIDIZI WA MRUNDI KAZE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top