• HABARI MPYA

  Tuesday, January 12, 2021

  TANZANIA YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA DRC MECHI YA KIRAFIKI LEO KUJIANDAA NA FAINALI ZA CHAN

  Na Asha Said, DAR ES SALAAM
  TANZANIA imelazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa kirafiki maalum uliotumika kumuaga beki wa Azam FC, Aggrey Morris jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
  Aggrey Morris akiwa anacheza mechi yake ya mwisho na jezi yenye bendera ya nchi yake tangu mwaka 2009 alicheza kwa dakika sita kabla ya kumpisha chipukizi, Carlos Protas aliyemalizia mchezo.
  Wageni, DRC walitangulia kwa bao la Kayele Kalala dakika ya 18 kwa shuti kali la umbali wa mita 22 lililompita kipa mkongwe, Juma Kaseja, lakini kiungo mshambuliaji wa Azam FCm Ayoub Lyanga akaisawazishia Stars dakika ya 51 akimalizia krosi nzuri ya mtokea benchi Ditram Nchimbi.


  Huo ulikuwa mchezo maalum wa timu zote kujiandaa na Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), michuano inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee zitakazofanyika Cameroon kuanzia Januari 16 hadi Februari 7, 2021.
  Tanzania imepangwa Kundi D pamoja na Zambia, Guinea na Namibia na DRC ipo Kundi B pamoja na Libya, Kongo-Brazaville na Niger wakati Kundi A kuna Cameroon, Mali, Burkina Faso na Zimbabwe, na Kundi C lina mabingwa watetezi Morocco, Rwanda, Uganda na Togo.
  Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Juma Kaseja/Aishi Manula dk46, Shomari Kapombe, Yassin Mustapha/Edward Manyama dk46, Ibrahim Ame, Aggrey Morris/Carlos Protas dk6, Said Ndemla/ Baraka Majogoro dk84, Ayoub Lyanga/Farid Mussa dk55, Feisal Salum, Adam Adam/Yusuph Mhilu dk46, Lucas Kikoti/ Israel Mwenda dk84 na Deus Kaseke/Ditram Nchimbi dk46.
  DRC; Ley Matampi, Issam Mpeko, Luzolo Ernest, Enoch Inonga, Nathan Idumba, Amede Masasi, Philipe Kinzumbi/Likute Luezi dk70, Mika Miche Miche, Fiston Mayele/Djuma Shaaban dk70, Karim Kiekie/Beta Tumetuka dk70 na Glody Lilepo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA DRC MECHI YA KIRAFIKI LEO KUJIANDAA NA FAINALI ZA CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top