• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 08, 2021

  MIRAJ ATHUMANI ‘MADENGE’ APIGA MBILI SIMBA SC YAICHAPA CHIPUKIZI 3-1 KOMBE LA MAPINDUZI

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  SIMBA SC imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Chipukizi FC ya Pemba kwenye mchezo wa Kundi B jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Pongezi kwake Miraj Athumani ‘Madenge’ aliyefunga mabao mawili dakika ya 53 na 83 baada ya mshambuliaji mwingine, Mnyarwanda Meddie Kagere kufunga la kwanza dakika ya 45 kufuatia Chipukizi kutangulia kwa bao la Fakhi Mwalimu Sharrif dakika 36.
  Mchezo wa Kundi A baina ya vigogo, Yanga SC ya Dar es Salaam na Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi inafuatia hivi sasa hapo hapo Uwanja wa Amaan.


  MAKUNDI
  Kundi B; Simba SC, Mtibwa Sugar, Chipukizi FC.
  Kundi A; Yanga SC, Namungo FC, Jamhuri FC
  Kundi C; Azam FC, Malindi FC, Mlandege FC
  MATOKEO NA RATIBA 
  Januari 5, 2021
  Yanga SC 0-0 Jamhuri
  Mtibwa Sugar 1-0 Chipukizi
  Januari 6, 2021
  Malindi FC 0-0 Mlandege
  Januari 7, 2021
  Azam FC 1-1 Mlandege FC
  Januari 8, 2021
  Simba SC 3-1 Chipukizi
  Yanga SC v Namungo FC
  Januari 9, 2021
  Azam FC v Malindi FC
  Januari 10, 2021
  Jamhuri FC v Namungo FC
  Simba SC v Mtibwa sugar
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MIRAJ ATHUMANI ‘MADENGE’ APIGA MBILI SIMBA SC YAICHAPA CHIPUKIZI 3-1 KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top