• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 14, 2021

  KIKOSI CHA TAIFA STARS CHAENDA CAMEROON FAINALI ZA CHAN 2021, KUFUNGUA DIMBA NA ZAMBIA JUMANNE

  KIKOSI cha Taifa Stars kimeondoka usiku wa kuamkia leo kwenda Cameroon kwa ajili ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zinazotarajiwa kuanza Jumamosi ya Januari 16 hadi Februari 7, 2021.
  Taifa Stars iliyopangwa Kundi D, itafungua dimba na Zambia Januari 19, yaani Jumanne ijayo Uwanja wa Limbe kabla ya kumenyana na Namibia Januari 23 na kumaliza na Guinea Uwanja wa Reunification, Douala Januari 27.  KUNDI A: Cameroon, Mali, Burkina Faso, Zimbabwe | KUNDI B: Libya, DRC, Kongo, Niger | KUNDI C: Morocco, Rwanda, Uganda, Togo | KUNDI D: Tanzania, Zambia, Guinea, Namibia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIKOSI CHA TAIFA STARS CHAENDA CAMEROON FAINALI ZA CHAN 2021, KUFUNGUA DIMBA NA ZAMBIA JUMANNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top