• HABARI MPYA

  Saturday, January 16, 2021

  SAMATTA AREJEA NA MOTO WAKE WA MABAO, AIPELEKA FENERBAHCE ROBO FAINALI YA KOMBE LA UTURUKI

  BAADA ya kuwa nje tangu Novemba mwaka jana, Nahodha wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta juzi alirejea uwanjani na kuisaidia klabu yake, Fenerbahce kutinga Robo Fainali ya Kombe la Uturuki kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Kasımpasa.
  Na ni Samatta, mchezaji wa zamani wa African Lyon, Simba SC za nyumbani, Dar es Salaam, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), KRC Genk ya Ubelgiji na Aston Villa ya England aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 51 akimalizia pasi ya beki Caner Erkin.
  Samatta aliumia Novemba 7, Fenerbahce ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Konyaspor katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki na nafasi yake kuchukuliwa na Ferdi Erenay Kadioglu dakika ya 69.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AREJEA NA MOTO WAKE WA MABAO, AIPELEKA FENERBAHCE ROBO FAINALI YA KOMBE LA UTURUKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top