• HABARI MPYA

  Friday, January 08, 2021

  SIMBA SC WAPANGWA KUNDI MOJA NA AL AHLY, AS VITA NA EL MERREIKH LIGI YA MABINGWA AFRIKA

  MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamepangwa Kundi A pamoja na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na El Marreikh ya Sudan katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
  TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yenye washambuliaji Watanzania, Thomas Ulimwengu na Eliud Ambokile imepangwa Kundi B na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Al Hilal ya Sudan na CR Belouizdad ya Algeria.
  Wydad Casablanca yenye kiungo mshambuliaji Mtanzania, Simon Msuva imepangwa Kundi C na Horoya AC ya Guinea, Petro Atletico ya Angola na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.


  Vigogo wa Tunisia, Esperance wao wamepangwa Kundi D na vigogo wa Misri, Zamalek, MC Algiers ya Algeria na Teungueth ya Senegal.
  Simba SC itaanzia ugenini na AS Vita Februari 12 mjini Kinshasa kabla ya kuja kuwakabilia Al Ahly Dar es Salaam Februari 23 na kukamilisha mzunguko wa kwanza kwa mchezo mwingine wa ugenini dhidi ya El Merreikh nchini Sudan Machi 5.
  Raundi ya pili wataanzia nyumbani dhidi ya El Merreikh Machi 16, kabla ya kuwaalika AS Vita Aprili 2 na kwenda kukamilisha mechi zake nchini Misri kwa kumenyana na Al Ahly Aprili 9.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAPANGWA KUNDI MOJA NA AL AHLY, AS VITA NA EL MERREIKH LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top