• HABARI MPYA

  Friday, January 15, 2021

  YANGA SC YAMSAJILI NYOTA WA ZAMANI WA MAMELODI SUNDWONS YA AFRIKA KUSINI, MRUNDI ABDUL RAZAK FISTON


  KLABU ya Yanga imetangaza kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Fiston Abdul Razak kutoka ENPPI ya Misri, hilo likiwa ingizo jipya la tatu katika dirisha dogo baada ya Mrundi mwenzake, Said Ntibanzokiza na beki mzawa, Dickson Job.
  Fiston mwenye umri wa miaka 27 ana uzoefu mkubwa kisoka na aliibukia akademi ya Lydia Ludic mwaka 2009 kabla ya kwenda Rayon Sports ya Rwanda, 2012, Diables Noirs 2013 ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sofapaka ya Kenya 2014.
  Mwaka 2017 alikwenda Mamelodi Sundowns, ambayo baadaye ilimtoa kwa mkopo Bloemfontein Celtic, zote za Afrika Kusini, ambako hakukaa sana akaenda Primiero de Agosto ya Angola 2017, Al-Zawraa ya Iraq mwaka 2018, JS Kabylie ya Algeria 2019 na ENPPI SC mwaka jana.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAMSAJILI NYOTA WA ZAMANI WA MAMELODI SUNDWONS YA AFRIKA KUSINI, MRUNDI ABDUL RAZAK FISTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top