• HABARI MPYA

  Sunday, January 17, 2021

  NAIBU WAZIRI WA ZAMANI WA MICHEZO, JUMA NKAMIA APITISHWA KUWANIA UENYEKITI WA KLABU YA SIMBA

  KAMATI ya uchaguzi ya Simba SC imempitisha aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa na Mbunge wa zamani wa jimbo la Chemba, Juma Nkamia kugombea Uenyekiti wa klabu hiyo.
  Katika uchaguzi huo mdogo uliopangwa kufanyika Februari 7, mwaka huu, Nkamia aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi wa Simba awali, atapambana na Mbunge wa zamani wa Kilwa, Murtaza Mangungu.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Simba SC, Boniface Lihamwike amesema wawili hao ndio watakaopambana katika uchaguzi huo mdogo kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti, Swedi Nkwabi Septemba 14, mwaka 2019.
  Na hiyo baada ya kuenguliwa kwa Mbunge wa jimbo la Mlalo, Lushoto mkoani Tanga, Rashid Abdallah Shangazi na Bittony Innocent Mkwakisu na Khamis Omar Mtika wakienguliwa.


  Mjumbe wa Bodi ya Wakurungenzi ya Simba, Mwina Kaduguda aliteuliwa kuwa Kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo baada Mkwabi kujiuzulu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAIBU WAZIRI WA ZAMANI WA MICHEZO, JUMA NKAMIA APITISHWA KUWANIA UENYEKITI WA KLABU YA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top