• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 25, 2021

  BEKI ERASTO NYONI AREJESHWA NYUMBANI KUTOKA KAMBI YA TAIFA STARS NCHINI CAMEROON KWA SABABU ZA KIAFYA

  BEKI Erasto Edward Nyoni amerejeshwa nyumbani kutoka kambi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars huko Cameroon kwa sababu Kiafya.
  Nyoni, beki wa klabu bingwa Tanzania, Simba alichelewa kujiunga na timu hiyo kwa madai ya matatizo ya kifamilia lakini hata baada ya kujiunga na timu ikiwa mjini Limbe hajacheza mechi yotote kati ya mbili za awali Taifa Stars ikifungwa 2-0 na Zambia na kushinda 1-0 dhidi ya Namibia. 
  Anarejeshwa nyumbani kuelekea mechi ya mwisho ya Kundi D ya Taifa Stars dhidi ya Guinea ambayo wanatakiwa kushinda ili kusonga mbele. 


  Zambia na Guinea kila moja ina pointi nne, zikifuatiwa na Tanzania yenye pointi tatu, wakati Namibia ambayo itamaliza Zambia haina pointi inashika mkia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BEKI ERASTO NYONI AREJESHWA NYUMBANI KUTOKA KAMBI YA TAIFA STARS NCHINI CAMEROON KWA SABABU ZA KIAFYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top