• HABARI MPYA

  Monday, January 11, 2021

  SIMBA SC WAICHAPA NAMUNGO FC 2-1 AMAAN NA KUWAFUATA YANGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

  MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC wamefanikiwa kwenda fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Namungo FC Uwanja wa Amaan, Zanzibar usiku wa leo.
  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na washambuliaji wake Mnyarwanda, Meddie Kagere dakika ya saba na Miraj Athumani ‘Madenge’ dakika ya 41, wakati la namungo FC limefungwa na Mghana, Steven Sey dakika ya 88.
  Sasa Simba SC watakutana na mahasimu wao wa jadi, Yanga SC Jumatano usiku katika fainali hapo hapo Uwanja wa Amaan.
  Hii inakuwa mara ya nane kwa Simba SC kuingia fainali ya michuano hiyo tangu ianzishwe mwaka 2007 wakiwa wametwaa Kombe hilo mara tatu, 2008, 2011 na 2015 huku 2012, 2014, 2017, 2019 na 2020 wakitoka patupu.
  Kukutana na Yanga SC katika Fainali hii itakuwa mara ya pili baada ya mwaka 2011 Simba waliposhinda 2-0, mabao ya Shijja Mkina na Mussa Mgosi hapo hapo Uwanja wa Amaan.


  ORODHA YA MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI
  Mwaka            Bingwa Mshindi wa Pili
  2007 Yanga SC Mtibwa Sugar 
  2008 Simba SC Mtibwa Sugar
  2009 Miembeni        KMKM
  2010 Mtibwa Sugar         Ocean View
  2011 Simba SC  Yanga SC
  2012 Azam FC          Simba SC
  2013 Azam FC    Tusker FC
  2014 KCCA        Simba SC
  2015 Simba SC Mtibwa Sugar
  2016 URA Mtibwa Sugar
  2017 Azam FC Simba SC
  2018 Azam FC URA FC
  2019 Azam FC Simba SC 2-1 
  2020 Mtibwa Sugar         Simba SC 1-0
  2021 ??? ???
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAICHAPA NAMUNGO FC 2-1 AMAAN NA KUWAFUATA YANGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top