• HABARI MPYA

  Jumapili, Januari 31, 2021

  SIMBA SC WATWAA KOMBE LA KWANZA 2021 BAADA YA KUTOA SARE YA 0-0 NA TP MAZEMBE YA DRC LEO DAR

  WENYEJI, Simba SC wametwaa taji la Simba Super Cup licha ya kulazimishwa sare ya 0-0 na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kwa matokeo hayo Simba SC inamaliza na pointi nne kufuatia ushindi wa 4-1 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Al Hilal ya Sudan Jumatano hapo hapo kwa Mkapa.
  Hilal ya Sudan imemaliza nafasi ya pili kwa pointi zake tatu baada ya kuichapa Mazembe 2-1 Ijumaa.


  Kiungo kutoka Msumbiji, Luis Miquissone aliteuliwa Mchezaji Bora wa Mechi ya leo na kupewa Sh 500,000.
  Kiungo Mzambia, Larry Bwalya aliteuliwa Mchezaji Bora wa Mashindano, wakati Mfungaji Bora ni winga Mghana, Bernard Morrison aliyepachika mabao mawili na Kipa Bora Beno Kakolanya wote waliapata Sh. Milioni 2 kila mmoja. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC WATWAA KOMBE LA KWANZA 2021 BAADA YA KUTOA SARE YA 0-0 NA TP MAZEMBE YA DRC LEO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top