// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ZIDANE AWAKUSANYA MASHUJAA WENZAKE WA KOMBE LA DUNIA UFARANSA 1998 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ZIDANE AWAKUSANYA MASHUJAA WENZAKE WA KOMBE LA DUNIA UFARANSA 1998 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, December 02, 2014

    ZIDANE AWAKUSANYA MASHUJAA WENZAKE WA KOMBE LA DUNIA UFARANSA 1998

    MWANASOKA bora wa zamani wa Dunia, Zinadine Zidane amekutana na mashujaa wenzake walioipa Ufaransa Kombe la mwaka 1998 na kupiga nao picha ya pamoja ya kumbukumbu wakiwa wameizunguka meza kwa chakula cha usiku.
    Zinedine Zidane ameposti picha hiyo na kikosi cha ubingwa wa Kombe la dunia mwaka  mjini Paris jana usiku, akiwa na nyota wenzake wa enzi hizo kama Laurent Blanc, Fabien Barthez, Didier Deschamps na Lilian Thuram.
    "Ufaransa 98 mjini Paris! Chakula cha usiku na marafiki wakubwa na wachezaji ndani ya Paris!" ameandika Zidane kama maelezo ya picha hiyo katika akaunti yake ya Instagram.
    Zinedine Zidane posted this picture on his Instagram account of players from France's 1998 World Cup-winning squad at a reunion in Paris. (Front row, from left) Laurent Blanc, Bixente Lizarazu, Zidane, Christian Karembeu, Bernard Diomede, Ludovic Giuly. Back row (from right) Lilian Thuram, Bernard Lama, Frank Leboeuf, Didier Deschamps, Christophe Dugarry, Sabri Lamouchi, Fabien Barthez.
    Zinedine Zidane ameposti hii picha kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa na wachezaji wenzake walioipa Ufaransa Kombe la Dunia mwaka 1998 mjini Paris. (Mbele, kutoka kushoto) Laurent Blanc, Bixente Lizarazu, Zidane, Christian Karembeu, Bernard Diomede, Ludovic Giuly. Nyuma kutoka kulia) Lilian Thuram, Bernard Lama, Frank Leboeuf, Didier Deschamps, Christophe Dugarry, Sabri Lamouchi na Fabien Barthez.
    The France team prior to the 1998 World Cup final with Brazil, which they won 3-0. (From top left: Zinedine Zidane, Marcel Desailly, Frank Leboeuf, Lilian Thuram, Stephane Guivarc'h, Emmanuel Petit; bottom left, Christian Karembeu, Youri Djorkaeff, Didier Deschamps, Fabien Barthez, Bixente Lizarazu)
    Kikosi cha Ufaransa kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 1998 kwa kuifunga Brazil fainali mabao 3-0. (Juu kutoka kushoto: Zinedine Zidane, Marcel Desailly, Frank Leboeuf, Lilian Thuram, Stephane Guivarc'h, Emmanuel Petit; waliochuchumaa kutoka kushoto ni Christian Karembeu, Youri Djorkaeff, Didier Deschamps, Fabien Barthez na Bixente Lizarazu)

    Zidane alikuwa nyota wa timu hiyo iliyotamba katika fainali zilizofanyika nyumbani wakiifunga Brazil 3-0 mechi ya mwisho na kutwaa taji lao la kwanza na pekee la Kombe la Dunia.
    Zizou, aliyefunga mabao mawili kwenye fainali pichani ameketi na mabeki Bixente Lizarazu na Blanc, ambaye kwa sasa ni kocha wa Paris Saint-Germain.
    Katika bega lake lingine kuna kiungo Christian Karembeu, anayefanya kazi Olympiacos ya Ugiriki, Bernard Diomede na Ludovic Giuly, ambaye hakuwemo kwenye kikosi cha 1998.
    Nyuma yao kuna beki Thuram, kipa wa pili Bernard Lama, Leboeuf, Deschamps, Christophe Dugarry, Sabri Lamouchi, ambaye hakuwemo kwenye kikosi cha mwisho na Barthez.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZIDANE AWAKUSANYA MASHUJAA WENZAKE WA KOMBE LA DUNIA UFARANSA 1998 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top