MABINGWA watetezi, Yanga SC wamelikaribia taji la tano mfululizo la Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya TRA United jioni ya leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Shujaa wa Yanga SC leo ni winga Mganda, Allan Jolly Okello ‘Star Boy’ aliyefunga mabao yote hayo matatu peke yake dakika za 27, 51 kwa penalti na 57.
Kwa ushindi huo, Yanga SC wanafikisha pointi 72 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi mbili Zaidi ya wapinzani wao, Simba SC kufuatia timu zote kucheza mechi 29 kuelekea mechi za mwisho za msimu Jumanne.
Kwa upande wao, TRA United baada ya kupoteza mchezo wa leo inabaki na pointi zake 42 kufuatia kucheza mechi 29 pia wakisalia pia katika nafasi ya tano.



.png)
0 comments:
Post a Comment