• HABARI MPYA

  Tuesday, December 02, 2014

  MANDAWA AMBWAGA OWINO TUZO YA MCHEZAJI BORA LIGI KUU NOVEMBA

  MSHAMBULIAJI wa Kagera Sugar ya Bukoba, Rashid Mandawa amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mwezi Novemba mwaka huu ambapo atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja.
  Mandawa ambaye kwa mwezi huo alichuana kwa karibu na mshambuliaji Fulgence Maganda wa Mgambo Shooting ya Tanga na Nahodha wa Simba, Joseph Owino atakabidhiwa zawadi yake na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom.
  Hafla ya kukabidhi zawadi hiyo inatarajiwa kufanyika wakati wa mechi ya raundi ya nane ya ligi hiyo kati ya Simba na Kagera Sugar itakayochezwa Desemba 26 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Joseph Owino katikati ameangushwa na Rashid Mandawa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Novemba


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANDAWA AMBWAGA OWINO TUZO YA MCHEZAJI BORA LIGI KUU NOVEMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top