• HABARI MPYA

  Tuesday, December 02, 2014

  KOZI YA UKUFUNZI WA UTAWALA YA FIFA SASA MACHI

  SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limesogeza mbele kozi ya ukufunzi ya utawala wa mpira wa miguu iliyokuwa ifanyika Desemba mwaka huu jijini Dar es Salaam.
  Kwa mujibu wa FIFA, kozi hiyo sasa itafanyika Machi mwakani katika tarehe itakayotangazwa baadaye.
  TFF imepokea maombi ya zaidi ya washiriki 40 kwa ajili ya kozi hiyo itakayoshirikisha washiriki 30. Kutokana na maombi kuzidi idadi ya nafasi zilizopo, FIFA itafanya mchujo wa washiriki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOZI YA UKUFUNZI WA UTAWALA YA FIFA SASA MACHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top