• HABARI MPYA

  Saturday, December 13, 2014

  LAMPARD AFUNGA BAO LA 175 LIGI KUU ENGLAND MAN CITY IKIILAZA 1-0 LEICESTER

  BAO pekee la kiungo mkongwe, Frank Lampard limeipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya Leicester City Uwanja wa King Power katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo.
  Kiungo huyo wa zamani wa Chelsea, alifunga dakika ya 40 ambalo linakuwa bao lake la 175 katika historia yake ya kucheza Ligi Kuu ya England na kumfikia nyota wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry. 
  Katika mchezo wa leo, City iliyomkosa mshambuliaji wake tegemeo, Sergio Aguero ambaye ni majeruhi, ilipata pigo lingine baada ya beki Vincent Kompany kuumia dakika ya 74.
  Kikosi cha Leicester kilikuwa; Hamer, Simpson, Wasilewski, Morgan, Konchesky, Mahrez, King, Cambiasso, Drinkwater/Knockaert dk79, Schlupp/Ulloa dk64 na Vardy/Powell dk73.
  Manchester City; Hart, Sagna, Kompany/Demichelis dk77, Mangala, Clichy, Fernando, Lampard/Milner dk60, Nasri, Toure, Silva na Pozo/Navas dk74.
  Lampard yet again came up good for Manchester City as he gave them the lead in the 40th minute
  Lampard yet again came up good for Manchester City as he gave them the lead in the 40th minute

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2872643/Leicester-City-0-1-Manchester-City-Frank-Lampard-strike-settles-Premier-League-match-Vincent-Kompany-goes-injured.html#ixzz3LndmcuC1 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LAMPARD AFUNGA BAO LA 175 LIGI KUU ENGLAND MAN CITY IKIILAZA 1-0 LEICESTER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top