• HABARI MPYA

  Saturday, December 13, 2014

  CHELSEA YANG'ARA LIGI KUU ENGLAND

  CHELSEA imeichapa mabao 2-0 Hull City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge, London jioni ya leo. 
  Eden Hazard alifunga bao la kwanza dakika ya saba kwa kichwa akiunganisha krosi ya Oscar, kabla ya Tom Huddlestone wa Hull kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 60 kwa kumchezea rafu Filipe Luis.
  Diego Costa akaifungia The Blues bao la pili dakika ya 68, ambalo linakuwa la kwanza ndani ya mechi nne na la 12 msimu huu.
  Ushindi huo, unaifanya timu hiyo ya kocha Mreno, Jose Mourinho ipae kileleni kwa pointi tatu zaidi, dhidi ya mabingwa watetezi, Manchester City.

  Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Luis, Mikel, Matic, Willian, Oscar, Hazard na Costa.
  Hull's Tom Huddlestone keeps his feet while Oscar takes the aerial route to a bouncing ball
  Hull's Tom Huddlestone keeps his feet while Oscar takes the aerial route to a bouncing ball
  Ivanovic (left) and Matic (right) get in on the celebrations after Costa hits the back of the net yet again
  Ivanovic (left) and Matic (right) get in on the celebrations after Costa hits the back of the net yet again

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2872741/Chelsea-2-0-Hull-Eden-Hazard-strikes-early-sets-Diego-Costa-Blues-hit-cruise-control-against-10-man-Tigers.html#ixzz3LngPBoIr 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YANG'ARA LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top