// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); IVORY COAST, MALI NA CAMEROON KUNDI MOJA AFCON, ZAMBIA YAPEWA DRC NA TUNISIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE IVORY COAST, MALI NA CAMEROON KUNDI MOJA AFCON, ZAMBIA YAPEWA DRC NA TUNISIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, December 03, 2014

    IVORY COAST, MALI NA CAMEROON KUNDI MOJA AFCON, ZAMBIA YAPEWA DRC NA TUNISIA

    VIGOGO Ivory Coast, Cameroon na Mali wamepangwa kundi moja, D Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mapema mwakani, wakati Zambia imepangwa Kundi B pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Cerpe Verde na Tunisia.
    Afrika Kusini, au Bafana Bafana imejikuta katika kundi la vigogo kuelekea Fainali hizo za 2015 baada ya droo iliyopangwa leo usiku.
    Vijana wa Shakes Mashaba wamewekwa Kundi C pamoja na Algeria na Ghana, ambao wote walikuwepo kwenye Kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil. Timu nyingine katika kundi hilo ni Senegal. 
    Upangwaji wa makundi hayo ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Hicham El Amrani aliyesaidiwa na kiungo wa zamani wa kimataifa wa Misri, Mohamed Aboutreika, nyota wa zamani wa Cameroon aliyecheza Kombe la Dunia 1994 na 1998, Alphonse Tchami na kocha wa Afrika Kusini, Ephraim 'Shakes' Mashaba.
    Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 17 hadi Februari 8 Equatorial Guinea.

    MAKUNDI YOTE AFCON 2015
    Kundi A - Equatorial Guinea, Kongo, Gabon, Burkina Faso
    Kundi B - Zambia, DRC, Cape Verde, Tunisia
    Kundi C - Ghana, Senegal, Afrika Kusini, Algeria
    Kundi D - Ivory Coast, Mali, Cameroon, Guinea
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IVORY COAST, MALI NA CAMEROON KUNDI MOJA AFCON, ZAMBIA YAPEWA DRC NA TUNISIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top