• HABARI MPYA

  Wednesday, December 03, 2014

  KOCHA MSERBIA ORLANDO PIRATES AJIUZULU BAADA YA KIPIGO JANA

  Na Mwandishi Wetu, SOWETO
  KOCHA wa Orlando Pirates, Vladimir Vermezovic (pichani kulia) amethibitisha kujiuzulu katika klabu hiyo kufuatia kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Maritzburg United jana, zikiwa ni siku chaxhe kabla hawajakutana na wapinzani wao wa Soweto, Kaizer Chiefs.
  Kocha huyo Mserbia aliwasilisha kujiuzulu kwake leo asubuhi, ambako kumekubaliwa na bosi wa Pirates, Dk Irvin Khoza.
  Kuondoka kwake kunahitimisha miezi tisa ya kufanya kwake kazi katika klabu hiyo ambayo ilitwaa Kombe la Nedbank mwezi Mei, lakini matokeo mabaya kwenye Ligi kuanzia mwishoni mwa msimu uliopita na msimu huu, yanawatenganisha.
  Anaondoka akiacha mataji ya Kombe la Nedbank na Carling Black Label Orlando Pirates na zaidi kushindwa kumudu presha ya mashabiki ndiko kunamfanya Vermezovic aondoke baada ya kipigo cha Maritzburg, wakati alitakiwa kuiunganisha timu katika wakati mgumu baada ya kifo cha kipa Senzo Meyiwa.
  Vermezovic pia amewahi kufanya kazi Kaizer Chiefs kwa miaka mitatu kuanzia 2009 hado 2012, ambako alishinda taji la Telkom Knockout mara mbili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA MSERBIA ORLANDO PIRATES AJIUZULU BAADA YA KIPIGO JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top