// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BILA RONALDO, BALE NA BENZEMA REAL MADRID YAUA 5-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BILA RONALDO, BALE NA BENZEMA REAL MADRID YAUA 5-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, December 03, 2014

    BILA RONALDO, BALE NA BENZEMA REAL MADRID YAUA 5-0

    LICHA ya kucheza bila nyota wake kibao wa kikosi cha kwanza kama, Cristiano Ronaldo, Karim Benzema, Gareth Bale na wengineo, Real Madrid imetinga 32 Bora ya Kombe la Mfalme baada ya kuifumua Cornella mabao 5-0 usiku huu Uwanja wa Bernabeu.
    Cornella walipoteza penalti dakika ya 15, kabla ya James Rodriguez kuwafungia wenyeji bao la kwanza dakika ya 16 na Isco kufunga la pili dakika ya 32.
    Mfungaji bora wa Kombe la Dunia aliye katika msimu wake wa kwanza Real, James akafunga tena bao la pili dakika ya 34, kabla ya bao la kujifunga la Borja Loez dakika ya 60.
    Jese Rodriguez akahitimisha ushindi huo mnono ambao unakuwa wa 17 mfululizo kwa Real Madrid kwa bao la dakika ya 77. Real inasonga mbele kwa ushindi wa jumla mabao 9-1, baada ya awali kushinda 4-1 ugenini. 
    Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Pacheco, Arbeloa, Varane/Llorente dk46, Nacho, Coentrao, Illarramendi, Khedira/Jese dk57, Medran, James, Isco na Hernandez.
    Cornella: Aberto, Pere, Borja, Pelegri, Israel, David, Luis, Gomez, Oscar Munoz/Trujillo dk56 na Gallar, Boniquet.
    James Rodriguez gives Real Madrid the lead as the Colombia international lifts the ball over Cornella goalkeeper Alberto
    James Rodriguez akiifungia bao la kwanza Real Madrid kwa kumtungua kipa Alberto
    Cornella' Alberto can do nothing to stop Isco's clever finish as the goalkeeper goes to ground to early
    Kipa wa Cornella, Alberto hakuweza kumzuia Isco kufunga

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2858139/Real-Madrid-5-0-Cornella-9-1-agg-James-Rodriguez-Isco-steal-Real-extend-winning-run-17-Jese-Rodriguez-marks-appearance-nine-months-goal.html#ixzz3KmNQ0GS3 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BILA RONALDO, BALE NA BENZEMA REAL MADRID YAUA 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top