• HABARI MPYA

  Wednesday, December 03, 2014

  MATA NA FELLAINI WAIPA USHINDI WA NNE MFULULIZO MAN UNITED ENGLAND

  KAMA ni mgonjwa, sasa kapona. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema, baada ya Manchester United kushinda mechi ya nne mfululizo Ligi Kuu ya England usiku huu.
  Timu hiyo ya kocha Mholanzi, Louis Van Gaal imeshinda mabao 2-1 Uwanja wa Old Trafford dhidi ya Stoke City na kurejea nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu.  
  Marouane Fellaini aliifungia Manchester United bao la kwanza dakika ya 21 kwa kichwa, kabla ya Steven Nzonzi kuisawazishia Stoke kwa shuti la mbali dakika ya 39 na Juan Mata kuwafungia bao la ushindi wenyeji kwa mpira wa adhabu dakika ya 59.
  United leo iliwakosa nyota wake majeruhi Wayne Rooney na Angel di Maria, na kwa ushindi huo ni dalili kwamba Van Gaal anaelekea kuanza ‘kupunga upepo’ Old Trafford.
  Kikosi cha Manchester United kilikuwa; De Gea, Valencia, Smalling, Rojo, Young, Fellaini, Carrick, Herrera/Fletcher dk86, Mata, Van Persie na Wilson/Falcao dk78.

  Stoke City; Begovic, Bardsley, Shawcross, Wilson, Pieters, Cameron, Nzonzi, Ireland/Arnautovic dk82, Krkic, Assaidi/Crouch dk77 na Diouf.
  United midfielder Juan Mata tries to shake off Stoke's Geoff Cameron in the opening exchanges
  Kiungo wa United, Juan Mata akijaribu kumhadaa Geoff Cameron wa Stoke CityFellaini celebrates putting United a goal up after 21 minutes at Old Trafford as Begovic sits on the turf
  Fellaini akishangilia baada ya kuifungia United bao la kwanza Uwanja wa Old Trafford, huku Begovic akiwa amejibweteka chini

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2857899/Manchester-United-2-1-Stoke-City-Juan-Mata-free-kick-gives-hosts-win-Marouane-Fellaini-header-cancelled-Steven-Nzonzi.html#ixzz3KmR7ybqL 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MATA NA FELLAINI WAIPA USHINDI WA NNE MFULULIZO MAN UNITED ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top