• HABARI MPYA

  Tuesday, December 02, 2014

  BEKI SIMBA SC AGOMBEWA NA POLISI, MWADUI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  POLISI ya Morogoro na Mwadui FC ya Shinyanga zimewasilisha barua kumuomba beki wa pembeni Miraj Adam wa Simba SC kwa mkopo.
  Polisi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inapambana na Mwadui FC, inayopigania kupanda Ligi Kuu pia kuwania huduma za beki huyo aliyetokea timu ya vijana ya Wekundu hao wa Msimbazi.
  Mwadui wanaamini wanaweza kumpata kwa urahisi beki huyo kwa sababu ya mahusiano mazuri ya kocha wao, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na klabu ya Simba SC.
  Miraj Adam kushoto anatakiwa na Polisi Moro na Mwadui ya Shinyanga baada ya kushushwa Simba B

  Julio ni mchezaji na kocha wa zamani wa Simba SC, ambaye pia ni mwanachama wa klabu hiyo aliyegombea nafasi ya Umakamu wa Rais katika uchaguzi wa katikati ha mwaka na kuangushwa na Geoffrey Nyange ‘Kaburu’. 
  Lakini Polisi nayo inaamini inaweza kumpata kwa urahisi beki huyo wa kulia, Miraj, kwa sababu inacheza Ligi Kuu kwa sasa na Morogoro si mbali sana na Dar es Salaam anakoishi mchezaji huyo.
  Kwa sasa, Miraj ameshushwa kikosi cha pili baada ya mechi saba za awali za Ligi Kuu, lakini Simba SC bado haijaamua kumtoa kwa mkopo hadi hapo itakapofanikisha kusajili mchezaji mwingine wa nafasi hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI SIMBA SC AGOMBEWA NA POLISI, MWADUI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top