• HABARI MPYA

  Monday, January 02, 2023

  POLISI TANZANIA YATOKA SULUHU NA RUVU SHOOTING MOSHI


  WENYEJI, Polisi Tanzania wamelazimishwa sare ya 0-0 na Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Kwa matokeo hayo katika mchezo wa 19 kwa kila timu, Polisi Tanzania inafikisha pointi 11, ingawa inaendelea kushika mkia ikizidiwa pointi mbili na Ruvu Shooting ya juu yake kwenye ligi ya timu 16.
  Ikumbukwe timu mbili zitateremka Daraja mwisho wa msimu na mbili zinakwenda kwenye mchujo wa kuwania kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLISI TANZANIA YATOKA SULUHU NA RUVU SHOOTING MOSHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top