• HABARI MPYA

  Wednesday, January 04, 2023

  ARSENAL YALAZIMISHWA SARE NA NEWCASTLE UNITED 0-0 EMIRATES


  WENYEJI, Arsenal wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumanne Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Pamoja na sare hiyo, Arsenal inaendelea kuongoza Ligi Kuu ya England kwa pointi zake 44 za mechi 17, ikiwazidi pointi nane mabingwa watetezi, Manchester City ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao Newcastle United baada ya sare hiyo wanafikisha pointi 35 katika mchezo wa 18 na kuendelea kushika nafasi ya tatu ikiizidi wastani wa mabao tú Manchester United ambayo imecheza mechi 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YALAZIMISHWA SARE NA NEWCASTLE UNITED 0-0 EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top