• HABARI MPYA

  Saturday, January 14, 2023

  MAN UNITED YATOKA NYUMA KUICHAPA MAN CITY 2-1


  WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester City katika mchezo was Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Haukuwa ushindi mwepesi, kwani Mashetani Wekundu walilazimika kutoka nyuma baada ya mahasimu wao wa Jiji kutangulia kwa bao la Jack Grealish dakika ya 60, kabla ya Bruno Fernandes kusawazisha dakika ya 78 na Marcus Rashford kufunga la ushindi dakika ya 82.
  Kwa ushindi huo, Manchester United wanafikisha pointi 38 na kusogea nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi moja tu Manchester City baada ya wote kucheza mechi 18.
  Ni Arsenal ndio wanaongoza Ligi Kuu kwa pointi zao 44 za mechi 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATOKA NYUMA KUICHAPA MAN CITY 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top