• HABARI MPYA

  Friday, January 20, 2023

  GEITA GOLD YATOKA SARE 1-1 NA POLISI TANZANIA 1-1 NYANKUMBU

   

  WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
  Geita walitangulia kwa bao la mshambuliaji Elias Maguri dakika ya 25, kabla ya Salum Ally kuisawazishia Polisi Tanzania dakika ya 90.
  Kwa matokeo hayo, Geita Gold imefikisha pointi 28, katika mchezo wa 21, ingawa inabaki nafasi ya tano ikizidiwa pointi 12 na Singida Big Stars ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao Polisi Tanzania wanafikisha pointi 15 katika mechi ya 21 na kusogea nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YATOKA SARE 1-1 NA POLISI TANZANIA 1-1 NYANKUMBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top