• HABARI MPYA

  Sunday, January 15, 2023

  SIMBA YATOKA NYUMA NA KUPATA SARE 2-2 NA CSKA MOSCOW


  TIMU ya Simba SC imetoka nyuma baada ya kipindi cha kwanza kwa mabao 2-0 na kupata sare ya 2-2 na CSKA Moscow ya Urusi katika mchezo wa kirafiki leo Abu Dhabi, Falme za Kiarabu (UAE).
  Baada ya CSKA Moscow kumaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza ikiwa inaongoza 2-0 kwa mabao ya 
  kwa mabao ya mshambuliaji Mrusi, Fedor Chalov dakika ya nne na winga Mparaguay, Jesús Medina dakika ya 25 kipindi cha pili Simba ilirejea vyema na kusawazisha  mabao hayo kupitia kwa mshambuliaji Habib Haji Kyombo dakika ya 52 na 76.
  Ulikuwa mchezo wa pili katika kambi yake ya UAE na wa pili chini ya kocha mpya, Mbrazil, Roberto Oliveira Goncalves do Carmo, maarufu kama Robertinho baada ya kuchapwa 1-0 Al Dhafra ya Madinat Zayed hapo hapo Abu Dhabi Ijumaa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YATOKA NYUMA NA KUPATA SARE 2-2 NA CSKA MOSCOW Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top