• HABARI MPYA

  Monday, January 09, 2023

  MLANDEGE YATINGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI


  WENYEJI, Mlandege wamefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Ibrahim Mkoko alianza kuifungia Namungo ya Ruangwa mkoani Lindi dakika ya saba, kabla ya Bashima Saite kuisawazishia Mlandege dakika ya 45.
  Sasa Mlandege itakutana na Singida Big Stars katika fainali, ambayo imeitoa Azam FC kwa kuichapa 4-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MLANDEGE YATINGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top