• HABARI MPYA

  Wednesday, January 04, 2023

  MAN UNITED YAIPIGA BOURNEMOUTH 3-0 OLD TRAFFORD


  WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya AFC Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumanne Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Man United yamefungwa na Casemiro dakika ya 23, Luke Shaw dakika ya 49 na Marcus Rashford dakika ya 86.
  Kwa ushindi huo, Man United inafikisha pointi 35 katika mchezo wa 17, ingawa inabaki nafasi ya nne, ikizidiwa wastani wa mabao mengi na Newcastle United ambayo pia imecheza mechi moja zaidi, wakati AFC Bournemouth inabaki na pointi zake 16 za mechi 18 nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAIPIGA BOURNEMOUTH 3-0 OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top