• HABARI MPYA

  Thursday, January 19, 2023

  MAN UNITED YATOA SARE 1-1 NA CRYSTAL PALACE


  TIMU ya Manchester United imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatano Uwanja wa Selhurst Park Jijini London.
  Kiungo Mreno, Bruno Fernandes alianza kuifungia Manchester United ya kocha Mholanzi, Erik ten Hag dakika ya 43, kabla ya Michael Olise kuisawazishia Crystal Palace dakika ya 90 na ushei.
  Man United inafikisha pointi 39 katika mchezo wa 19 baada ya sare hiyo na inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa tu wastani wa mabao na majirani, Manchester City yenye mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao, Crystal Palace wanafikisha pointi 23 na wao wanabaki nafasi ya 12 wakizidiwa pointi mbili na Aston Villa baada ya wote kucheza mechi 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATOA SARE 1-1 NA CRYSTAL PALACE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top