• HABARI MPYA

  Tuesday, January 31, 2023

  AL HILAL YAICHAPA AZAM FC 1-0 CHAMAZI


  BAO pekee la Mohamed Abdelrahman dakika ya 45 limeipa Al Hilal ya Sudan ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Azam FC katika mchezo wa kirafiki usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Ulikuwa mchezo wa wa pili wa kirafiki kwa Al Hilal ambayo imekuja nchini kuweka kambi ya kujiandaa na mechi yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini Februari 11 baada ya sare ya 1-1 na Namungo FC.
  Timu hiyo ya kocha Mkongo, Florent Ibenge itashuka tena dimbani Jumapili kumenyana na wenyeji wao, Simba SC Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AL HILAL YAICHAPA AZAM FC 1-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top