• HABARI MPYA

  Saturday, January 28, 2023

  SIMBA SC YAITOA COASTAL UNION KWA KUICHAPA 1-0 DAR


  BAO pekee la kiungo wa Kimataifa wa Mali, Sadio Kanoute dakika ya 56 limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. 
  Kwa matokeo hayo, Simba SC watakutana na wapinzani wengine kutoka Tanga, African Sports ambayo leo imewatoa wenyeji, New Dundee kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 0-0 Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAITOA COASTAL UNION KWA KUICHAPA 1-0 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top