• HABARI MPYA

  Thursday, January 05, 2023

  AZAM FC YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI


  TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Jamhuri katika mchezo wa Kundi A leo Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na Ismail Aziz dakika ya 34 na Abdul Suleiman ‘Sopu’ mawili yote kwa penalti dakika ya 52 na 81.
  Kwa matokeo hayo, Azam FC inamaliza mechi zake za Kundi A ikiwa na pointi nne, sawa na Malindi ambayo kwa kuizidiwa wastani wa mabao wanaungana na Jamhuri kuaga mashindano.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top