• HABARI MPYA

  Sunday, January 22, 2023

  HAALAND APIGA HAT TRICK YA NNE MAN CITY YASHINDA 3-0


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Pongezi kwa mfungaji wa mabao yote hayo, mshambuliaji wa Kimataifa wa Norway, Erling Haaland  aliyefunga mabao yote hayo, dakika ya 40 akimalizia pasi ya 40 Kevin De Bruyne, 50 kwa penalti na 54 akimalizia pasi ya Riyad Mahrez hiyo ikiwa hat-trick ya nne msimu.
  Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 45 katika mchezo wa 20, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tano na Arsenal ambao pia wana mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao Wolverhampton Wanderers baada ya kipigo cha leo wanabaki na pointi zao 17 za mechi 20 nafasi ya 17 kwenye ligi ya timu 20 ambayo mwisho wa msimu tatu zitateremka daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAALAND APIGA HAT TRICK YA NNE MAN CITY YASHINDA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top