• HABARI MPYA

  Friday, January 13, 2023

  YANGA YAMSAJILI MSHAMBULIAJI MZAMBIA KENNEDY MUSONDA


  MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania, Yanga SC wamemtambulisha mshambuliaji Mzambia, Kennedy Musonda kutoka Power Dynamos ya kwao kuwa mchezaji wao mpya.
  Huo unakuwa usajili wa pili tu katika dirisha hili dogo kwa Yanga, washindi wa mataji yote msimu uliopita pamoja na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) na Ngao ya Jamii ambayo pia wametwaa na msimu huu- baada ya kiungo Mzanzibari, Mudathir Yahya Abbas.
  Musonda mwenye umri wa miaka 28 pia amechezea timu za Green Eagles, Nakambala Leopards na Lusaka Dynamos zote za kwao na kwa sasa ni mchezaji wa timu ya taifa ya Zambia.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAMSAJILI MSHAMBULIAJI MZAMBIA KENNEDY MUSONDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top