• HABARI MPYA

  Friday, January 13, 2023

  SIMBA SC YACHAPWA 1-0 NA AL DHAFRA LEO ABU DHABI


  TIMU ya Simba SC ya Dar es Salaam imepoteza mechi yake ya kwanza ya kirafiki katika kambi yake fupi Falme za Kiarabu (UAE) baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Al Dhafra ya Madinat Zayed leo mjini Abu Dhabi.
  Simba SC ambayo sasa chini ya kocha Mbrazil, Roberto Oliveira Goncalves do Carmo, maarufu kama Robertinho aliyeiongoza timu kwenye mechi ya kwanza leo, itaerejea mazoezini kesho Dubai kabla ya Jumapili kucheza mwingine wa kirafiki dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YACHAPWA 1-0 NA AL DHAFRA LEO ABU DHABI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top