• HABARI MPYA

  Saturday, January 28, 2023

  KMC YAICHAPA COPCO 1-0 NA KUSONGA MBELE ASFC

  BAO pekee la mshambuliaji wa Kimataifa wa Burundi, Steve Nzigamasabo dakika ya 84 limeipa KMC ushindi wa 1-0 dhidi ya Copco FC ya Mwanza katika mchezo wa Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mechi nyingine za 32 Bora leo, African Sports ya Tanga imesonga mbele kwa ushindi wa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 na New Dundee Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma na Mbeya City imeitupa nje Mbeya Kwanza kwa kuichapa 1-0 Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
  Singida Big Stars imeitupa nje Ruvu Shooting kwa kuichapa 2-1 Uwanja wa LITI mjini Singida na wenyeji wengine, Geita Gold imeitoa Nzega United kwa kuichapa 1-0 Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YAICHAPA COPCO 1-0 NA KUSONGA MBELE ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top