• HABARI MPYA

  Tuesday, January 31, 2023

  SIMBA SC YAONGOZA KWA HAT-TRICK LIGI KUU


  KUELEKEA Raundi tisa za mwisho za Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba ndio inaongoza kwa kutoa waliofunga mabao matatu kila mmoja kwenye mechi moja, yaani hat-trick.
  Hadi sasa ndani ya Raundi 21 zilizochezwa, wachezaji wawili wa Simba, Nahodha John Bocco na kiungo Mrundi, Said Ntibanzokiza wamefunga hat-trick ikiwa klabu pekee ya Ligi Kuu kutoa wachezaji wawili waliofanya hivyo.
  Bocco amepiga hat-trick mbili hadi sasa na Ntibanzokiza moja, huku wengine waliofanya hivyo ni mshambuliaji Mkongo wa Yanga, Fiston Kalala Mayele wa Yanga na mshambuliaji Mzanzibari wa Namungo FC, Ibrahim Abdallah Mkoko.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAONGOZA KWA HAT-TRICK LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top