• HABARI MPYA

  Friday, January 13, 2023

  YANGA NA RHINO, SIMBA NA COASTAL NA AZAM FC V DODOMA JIJI ASFC


  MABINGWA watetezi, Yanga SC watamenyana na Rhino Rangers ya Tabora katika Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) mwishoni mwa mwezi huu Jijini Dar es Salaam.
  Washindi wa pili wa msimu uliopita, Coastal Union watakuwa wageni wa Simba, wakati Azam FC wataikaribisha Dodoma Jiji FC Jijini Dar es Salaam.
  Yanga wakiuvuka mtihani wa Rhino Rangers watakutana na kati ya Mashujaa na Tanzania Prisons, wakati Simba SC wakiitoa Coastal Union watakutana na mshindi kati ya New Dundee ya Dodoma na African Sports ya Tanga na Azam FC ikiing’oa Dodoma Jiji itacheza na mshindi baina ya Mapinduzi FC na Polisi Katavi.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NA RHINO, SIMBA NA COASTAL NA AZAM FC V DODOMA JIJI ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top