• HABARI MPYA

  Friday, January 06, 2023

  SIMBA SC YAAGA MAPINDUZI NA USHINDI WA 1-0 DHIDI YA KVZ


  WALIOKUWA mabingwa wa Kombe la Mapinduzi wamekamilisha ratiba ya mechi zao za mwaka huu kwa ushindi wa 1-0 usiku wa Alhamisi dhidi ya KVZ kwenye mchezo wa Kundi C Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo, chipukizi aliyeoandishwa kutoka timu ya vijana, Michael Joseph dakika ya 41 na sasa Simba wanamaliza na pointi tatu nyuma ya vinara, Mlandege wenye pointi nne ambao wanakwenda Nusu Fainali.
  KVZ iliyomaliza na pointi moja mkiani pia inaungana na Simba kuipa mkono wa kwaheri mapema tu michuano ya mwaka huu.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAAGA MAPINDUZI NA USHINDI WA 1-0 DHIDI YA KVZ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top