• HABARI MPYA

  Saturday, January 14, 2023

  BRIGHTON & HOVE ALBION YAITANDIKA LIVERPOOL 3-0 ENGLAND


  WENYEJI, Brighton & Hove Albion wametumia vyema Uwanja wa nyumbani, The Amex baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Liverpool FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
  Shujaa wa Brighton & Hove Albion alikuwa ni kiungo Solomon Benjamin March mawili aliyefunga manbao mawili dakika ya 46 na 53 kabla ya kumsetia Muingereza mwenzake, Danny Welbeck kufunga la tatu dakika ya 81.
  Kwa ushindi huo Brighton & Hove Albion wanafikisha pointi 30 na kusogea nafasi ya saba, wakati Liverpool inabaki na pointi zake 28 nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 18.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BRIGHTON & HOVE ALBION YAITANDIKA LIVERPOOL 3-0 ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top