• HABARI MPYA

  Friday, January 27, 2023

  MTIBWA SUGAR YASHINDA 4-0 NA KUSONGA MBELE ASFC


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wamefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Buhaya FC ya Bukoba leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
  Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Onesmo Mayaya mawili dakika ya 23 na 65 na Vitalis Mayanga mawili pia dakika ya 67 na 75.
  Matokeo ya mechi nyingine za leo, Polisi Tanzania imeitoa JKT Tanzania kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na Green Warriors imeitoa Mbuni FC kwa kuichapa 2-1 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YASHINDA 4-0 NA KUSONGA MBELE ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top