• HABARI MPYA

  Sunday, January 15, 2023

  ARSENAL YA MOTO, YAICHAPA SPURS 2-0 LONDON


  VINARA, Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London.
  Mabao ya Arsenal inayofundishwa na kocha Mikel Arteta yamefungwa na Hugo Lloris aliyejifunga dakika ya 14 na Martin Odegaard dakika ya 36 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 47 na kutanua uongozi wao kwa pointi nane zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 18.
  Kwa upande wao, Tottenham Hotspur baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 33 za mechi 19 nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YA MOTO, YAICHAPA SPURS 2-0 LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top